Je wajua kuwa ukiwekeza katika kilimo cha miti hakuna hasara?
Ukiwa na GreenProject waweza kutengeneza pensheni yako ambayo haiathiriwi na kikokotoo. Wala haikuhitaji wewe kuwa mwajiriwa ili uwe na uhakika wa pensheni. Wala huitaji kuomba kuchukua pensheni yako uliyoiandaa kwa mda mrefu. Na kwa uhakika pensheni yako hataathiriwa na mabadiliko ya kiuchumi (inflation) pia pensheni hiyo itakufanya kuweka alama na kuacha historia yako katika kumbukukmbu ya wanao jali.
Sasa nakujuza.
Maeneo ya vijijini ambako hatu wana mashamba ambayo hawaishi watu hukaa bila kuendelezwa licha ya kuwa na rutuba ya asili, vipindi viwili vya mvua na kutokuwa na wanyama waharibifu. Maeneo hayo huonekana hayana thamani (reject) kutokana na kutokuwepo huduma za msingi kama umeme, hospitali, maji, barabara nk. hivyo kama unataka kuyanunua muuzaji huuza kwa bei ndogo sana. Usishangae eneo hilo ukiambiwa kuuziwa heka moja kwa TSh. 200,000. Ndugu yangu hiyo ni fursa kwa mtu mwenye mtazamo wa mbele.
Nini cha Kufanya.
Tafuta mda, tembelea maeneo hayo yaliyo karibu na wewe, ulizia kama unaweza kupata maeneo hayo kwa gharama nafuu. Nina imani utapata maana wenye nayo hawana cha kuyafanyia zaidi ya kuyatunza kama kumbukumbu kurithishana kutoka kizazi na kizazi. Kisha anza kutunza akiba hakikisha unakuwa na uwezo wa kununua japo heka 10 sehemu hizo ambazo wengi husema hapafai kwa makazi (reject). Kisha andaa mradi kwa bei nafuu (Simple Project) wa kuwekeza hapo ambao baada ya miaka utapata mapato makubwa sana.
Mradi (Project).
MRADI | |
MAHITAJI | KIASI |
Viriba (Roller 3 ) @ 45,000 | 135,000.00 |
Udongo Mweusi Trip 2 | Free |
Mchanga robo trip | 15,000.00 |
Mbolea (Mboji) za, uozo wa miti, kuku, ngombe, mbuzi, n.k | Free |
Mbegu (pain, syplus, mitiki, n.k) | 50,000.00 |
Vifaa vya kumwagilizia (Watering Tank) | 20,000.0 |
Dawa ya wadudu (Past Sides) | 4,000.0 |
Jumla | 224,000 |
Kwa mahitaji hayo utaweza kuotesha miche kati ya 10,000 ampaka 20,000
Mambo ya kuzingatia kupunguza gharama.
- Hakikisha kitalu kiwe karibu na nyumbani ili kukurahisishia wewe kukimwagilizia maji kila asubuhi na jioni yaani kabla na baada ya wewe kutoka kazini. Ikiwa ni pamoja na kupalilia magugu kutoka katika kitalu hicho.
- Miche hiyo ilee kwa kipindi kisichopungua miezi minne ili iwe rahisi kwako kuisafirisha na kuipanda.
- Hakikisha unatengeneza ukaribu na ofisi za mazingira na mali asili ili kupata ushauri pale unapo uhitaji.
- Hakikisha unaandaa kitalu miezi minne kabla ya kipindi cha masika ili kupata urahisi kwa kupanda miche hiyo mara tu masika yatakapo anza
- Hakikisha unaipenda kazi hiyo kwa moyo yote na kuamini kuwa itaweza kukufanya kuwa bilionea
Matarajio
Kwa kuzitumia heka 10 unakuwa na uwezo wa kupanda anglau miche 10,000. Nini waweza kupata baada ya miaka 10 kama utafanikiwa kupanda miche 10,000.
MATARAJIO (EXPECTED REVENUE) | |
Jumla ya miti | 10000 |
Matarijio ya idadi ya mbao kwa kila mti | 4 |
Matarajio ya jumla ya mbao kutoka kwenye miti | 40,000.00 |
Kadirio la chini kwa kila ubao (Bei ya sasa) | 7,000.00 |
Kiasi cha fedha unachoweza kupata | Tsh. 280,000,000.00 |
Sasa Jiulize
- Sasa jaribu kulinganisha kwa miaka 30 unayomtumikia mwajiri unatarajia kupata pensheni kiasi gani?.
- Jiulize kama hiyo miti ungeiacha kwa miaka 30 ungevuna kiasi gani?.
- Je badala ya miche 10,000 ukipanda 200,000 baada ya miaka kumi unaweza kuwa katika kiwango gani?.
- Je ni lini unatarajia soko la mbao litaisha wakati biandamu tunazidi kuongezeka na majengo yanazidi kunyanyuliwa?
- Je ushajiuliza kuwa mradi huu unaweza kukugharimu kiasi gani?.
Faida za Mradi huu.
Kiuchumi.
- Msahara wako unatosha kuwa chanzo cha mtaji, hivyo huitaji kukopa ili kutunisha mtaji.
- Haikuhitaji kuwa mwajiriwa ili uweze kunufaika na pensheni hii, yoyote mwenye kipato cha kawaida anaweza kufanya
- Haihitaji usimamizi mkubwa (managerial follow up ) ili kufanikisha hili
- Kipato kutonaka na uwekezaji huu ni uhakika
- Kama umekatia hati miliki waweza kutumia kama dhamana kukopa benki kuendeleza biashara nyingine.
- Ni njia nzuri ya kulitunza na kuliendeleza shamba lako kwa vizazi na vizazi
Kimazingira na Kijamii
- Husaidia kutunza na kuviendeleza vyanzo vya maji
- Huchangia katika kupunguza mwedo kasi wa upepo na hivyo kuyatunza amazingira.
- Chanzo cha kutunza unyevunyevu aridhini na hivyo kuchangia katika uvukishaji ambao waweza kuwa chanzo cha mvua
- Kusaidia kupunguza kama sio kuondo kabisa maporomoko ya ardhi.
- Hupunguza carbon na kuongeza oxygen na hivyo kuchangia kupunguza tatatizo ya mabadiliko ya tabia ya nchi.
- Hutengeneza mazingira mazuri yenye muonekano mzuri kwa ajiri ya makazi ya viumbe hai.
- Hokoa vifo vingi vya wanyama na mimiea.
Mwisho
Ndugu yangu GreenProject ni sehemu sahihi ya wewe kujifunza kuwa bilionea huku ukiendelea kunufaika wewe na kunufaisha viumbe wengine. Kwa wale wasiokuwa na mda wa kuwekeza GreenProject tunaweza kukusaidia yafuatayo.
- Kuotesha kitalu
- Kupanda miche na kumwagilizia
- kuhamishia miche shambani
- kukukabithi shamba lenye utajiri mkubwa
- Na ukatulipa kidogokidogo, dhamana yako ni shamba lako
GreenProject tunasema tuoneshe shamba lako tukutengenezee zaidi ya pensheni yako maana kuwekeza kwenye kijani faida ni uhakikia.
Mawasiliano
E- Mail: info@cslso.or.tz, www.cslso.or.tz,
Comments are closed.