Akiongea na Wachimbaji wadogo wa Mgodi wa Ikuzi Wilayani BUKOMBE CPA .Sadick K.Rutenge kwa niaba ya Mamlaka ya Mapato (TRA) Mkoa wa Geita amesema ni mda wa wachimbaji wadogo kurasimisha biashara yao na kujisajili katika ofisi mbali mbali za serikali ikiwemo TRA ili kuhakikisha kila Mchimbaji anachangia katika pato la taifa kwa nafasi yake. Pia amesema wachimbaji wana nafasi ya kujisajili kupata kitambulisho cha Mjasiliamali kama mauzo yake ni chini ya Tsh. 4,000,000. 00 kwa mwaka au kujisajili na kupata TIN kama mauzo yake ni zaidi ya milioni nne kwa mwaka. Pia amesema kwa sasa taratibu za kujisajili zimerahisishwa. Kwa suala la kitambulisho mtu anaweza kujisajili mwenyewe kupitia MACHINGA APP au kutembelea Ofisi ya Afisa Biashara Wilaya ili kusajiliwa na usajili wa TIN , amemuomba mwenyekiti wa Mgodi wa Ikuzi kuwatambua watu wote waliopo katika mgodi huo. Baada ya kuwatambua TRA itakuja kuwasajili watu hao katika maeneo ya mgodi huo. Pia amesisitiza Ofisi ya TRA Bukombe kudumisha mahusiano na Afisa Madini Mkazi ili kubadilishana taarifa kwa ajili ya kurahisisha ukusanyaji makato. Taasisi zingine zilizo toa mada ni pamoja Benki ya CRDB, Benk ya NMB, TAKUKURU, GST, Tume ya Madini, Ofsi ya Mazingira, Halmashauri ya Wilaya na Ofisi ya Diwani.
Comments are closed.