Akijibu swali wakati wa Mahojiano na TCRA katika maadhimisho ya kilele cha mbio za mwenge na fursa kwa vijana walipo taka kujua faida za TEHAMA kwa TRA, CPA Sadick Rutenge amesema kuwa TRA inatumia TEHAMA katika shughuli mbalimbali zikiwa ni pamoja na
1. Usajili wa walipa kodi
2. Kutuma ritani za biashara
3. Kutoa mrejesho wa biashara
4. Kulipa kodi mbali mbali.
Pia ameongeza kuwa kwa sasa namna TRA inavyo fanya kazi huwezi kutenganisha matumizi ya TEHAMA na shughuli za TRA, maana TEHAMA imekuwa mkombozi na kutoa fursa kwa wafanya biashara kujihudumia wenyewe.
Comments are closed.