EMAIL US AT info@cslso.or.tz
CALL US NOW +255 767 710 320
DONATE NOW

KAMPUNI YA NDY GENERAL LIMITED KUKABIDHI VYUMBA VIWILI VYA MADARASA KATIKA SHULE YA MSINGI RUSHE KATA MABIRA WILAYANI KYERWA


Akimkabidhi Afisa Mtendaji kwa kijiji c ha Rushe MABATI 92, mwakilishi wa kampuni hiyo maarufu kama NDY GARMENTS iliopo mkoani Geita Ndg. Buruhan Kassimu Rutenge amesema Kampuni imetoa msaada huo baada ya Uongozi  wa Shirika la Community Serve and Life Survival Organization  kuitembelea Shule ya Msingi Rushe iliopo kata Mabira na kushuhudia watoto zaidi ya 100 wakijifunzia chini ya miti. Suala ambalo linakwamisha masomo wakati wa jua kali au mvua. Hivo shirika kwa kushirikiana na NDY GARMENTS kutoa msaada huo ili kusaidia watoto wasome kwa Amani.